Corona Break Experience.



Tulianza kuusikia kwenye radio, television, na kusoma mitandaoni, ugonjwa wa corona. Hatimaye umetugusa kwa namna moja ama nyingine. Idadi ya waathirika inaongezeka kwa kasi barani ulaya ukilinganisha na barani Afrika, huku nchi ya Afrika kusini ikiongoza kwa maambukizi. (mpaka post hii inapoandikwa.) 
kama nilivyoandika hapo juu hali ni mbaya kwa nchi za Ulaya. Spain na Italy hakuna watu mitaani, hasa ukizingatia ya kwamba wastani wa vifo kutokana na ugonjwa huu ni watu 350 ndani ya saa 24.

(Mwandishi wa blog bado mwanafunzi.)
Shuleni hali ilibadilika pale mwathirika wa kwanza aliporipotiwa kupatikana jijini Arusha. Hiyo ilikua tarehe 16 Aprili, na tarehe 17 Aprili Waziri mkuu Mheshimiwa Kassim M. alitangaza kufunga shule zote nchini.-ungetamani kufahamu tamko hili nililichukuliaje - "basi endelea kusoma post na uangalie video. "
Ila kama kawaida mzozo ulitokea shuleni, wapo waliafiki uamuzi na wengine hawakuafiki maamuzi haya, kila mtu kwa sababu zake.
Nikuulize, unadhani kwanini mgawanyiko huu ulitokea?

Ki-uharisia nilichotegemea kukuta mtaani sikukikuta, na hali ilikua tofauti na mtazamo wangu. Jambo hili lilinifanya kuandaa short experience yangu juu ya ugonjwa huu na hali nzima katika jamii.

Sasa chukua muda kutazama experience hio katika video hii fupi iliyotengenezwa na Bona_vision Production.
Bofya hapa chini kuangalia video.

Au bofya hapa ku-download video hii.