Vitu Vya Kufanya kwa Wanafunzi Likizo Hii Ya Corona.

Je, umejiuliza ni kwa namna gani unatakiwa kutumia muda wa likizo hii ya dharura? Katika blogpost hii nitakueleza mambo matano ambayo ni vyema kwa wanafunzi wote kufanya kipindi hiki cha likizo. Baadhi ya vitu utakua tayari unafanya kitu ambacho ni kizuri sana. Vitu hivyo ni kama ifuatavyo.
Mwandishi bado ni mwanafunzi. 
1. KUJISOMEA KWA BIDII.
Hiki ndicho kitu cha muhimu kabisa kufanya na nadhani unalifahamu hilo. Sasa unaweza kutengeneza ratiba itakayo kuongoza ukizingatia ya kwamba masomo au topics zinazokusumbua zinapata muda wa kutosha. Pia, kwa kuwa unasomea nyumbani jaribu kutenga ule muda ambao hakuna usumbufu kutoka kwa wanafamilia wengine. Kumbuka kwamba kusoma kwa bidii kipindi hiki itasaidia kuepuka usahaurifu, hakuna anaejua shule zitafunguliwa lini.
2. KUJIFUNZA KITU/VITU VIPYA.
Katika muda wako wa free unaweza kuutumia kujifunza stadi mpya au kufanya mazoezi zaidi ya vipaji ulivyonavyo. Unaweza kujifunza style mpya za kudance, au mazoezi ya kusoma vitabu kwa haraka (speed reading). Kwa mfano mimi napenda maswala ya content creation, natumia free time kutengeneza videos na blog posts kama hivi. Unaweza kutizama baadhi ya video hizo hapa.
3. KUFANYA KAZI ZA FAMILIA.
Ili kuepuka kuonekana kama mzigo katika familia chukua muda wako kufanya kazi za familia. Kazi hizo ni kama kupika, usafi wa mazingira na hata shughuli za kiuchumi kama kusimamia miradi ya familia. Sasa wasichana kwa wavulana kila mmoja anafahamu kazi gani akifanya wazazi watafurahi na hawatomchukulia kama mzigo nyumbani.
4. KUANGALIA MOVIE/SERIES.
Hii pia ni njia mojawapo ya kuondoa upweke. Ebu imagine Corona ingetokea wakati hakuna Internet! Ingekuaje? Kwa sasa unaweza kufuatilia movies na series uzipendazo mwanzo mwisho. Unaweza kutumia muda wako wa free kutizama movie uzipendazo. Kwa mfano mimi natazama series inayoitwa The Resident ya FOX. Unaweza kuniambia unatazama movie/series ipi kwenye comments katika page yetu ya Facebook.
5. KUPATA USINGIZI WA KUTOSHA.
Usingizi haukwepeki kwa namna yeyote. Sasa katika kipindi hiki jaribu kupata usingizi wa kutosha ili kuruhusu ubongo kufanya kazi vizuri. Tafiti zinaonesha ukosefu wa usingizi wa kutosha hudhoofisha mwili. Kumbuka kwamba baada ya kufungua shule kila shule itatembea kwa kasi ya hatari ili kufidia muda uliopotea, ukikosa usingizi wa kutosha utafungua shule ukiwa umechoka na utashindwa kwenda na speed ya waalimu.
BONUS.
Pia jaribu kujenga mazoea ya kusoma vitabu. Kama niljvyotangulia kusema ni bahati nzuri kwamba internet ipo na ina resources nyingi sana. Pakua vitabu uvipendavyo na usome.
Zingatia sana kupata taarifa kuhusu ugonjwa wa Corona kutoka katika vyombo sahihi kama Wizara ya Afya na vingine.
Ni hayo tu, endelea kutufuatilia katika page zetu za mitandao ya kijamii.