Matukio 10 Makubwa Kutoka Kwenye "My Life, My Purpose" Kitabu Cha Mkapa.


My Life My Purpose ni kitabu alichoandika hayati Benjamini W. Mkapa baada ya kustaafu Uraisi wake. Kitabu hiki alikizindua rasmi mwaka 2019 mbele ya raisi mstaafu J. Kikwete na raisi JP. Magufuli. Nakala ya kitabu hiki inapatikana katika vyanzo vyote vya uuzaji wa vitabu. 

Kupitia blog post hii tunaenda kuona yale matukio 10 yanayopatikana katika kitabu hicho. Kumbuka ya kwamba matukio makubwa ni mengi lakini tunayoenda kuyaona ni baadhi yake tu. 
Fahamu: B. Mkapa ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne. 

MATUKIO MUHIMU KUTOKA KWENYE KITABU. 
1. Baba yake B. Mkapa alikua mpishi msaidizi wa mission(misheni) ya Ndanda wakati wa ukoloni. 
2. Mama yake B. Mkapa hakujua kusoma wala kuandika lakini alikua na msimamo na mchango mkubwa katika elimu ya mwanae. 
3. Mwaka 1947, B. Mkapa akiwa na umri wa miaka 9 mama na bibi yake walihusishwa na tukio la kuleta ukame kijijini kwa kuzuia mvua. Hii ilipelekea kushikwa uchawi na kushushiwa kipigo kizito na wananchi, kilichopelekea kifo cha bibi yake! 
4. Kutoka darasa la wanafunzi 25 kijijini Lupaso, yeye na rafiki yake tu ndio walifanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari. 
5. Baba yake B. Mkapa alitegemea na alimuandaa mwanae kuwa Padre, Daktari au Mwalimu. "Soma inayofuata"
6. B. Mkapa alijiunga na Seminary ya St. Francis Pugu, lakini baadae alihama baada ya kuona hakuwa na wito wa upadre. Badala yake alijiunga na shule ya Ndanda ya Wamissionary ambako alianza maswala ya siasa.  
7. B. Mkapa alichukua shahada ya lugha na fasihi ya kiingereza huko Makerere University, Uganda. Pia alisomeshwa na serikali nchini Marekani katika chuo cha Columbia, alipoenda kubobea katika maswala ya Diplomasia. (Umri wa miaka 24)
8. Akiwa bado mtumishi wa serikali aliomba kwa hiari yake na kujiunga na jeshi, japo JK. Nyerere alikua hakubaliani na wazo hilo. 
9. Amethamini sana mchango wa JK. Nyerere katika Utumishi wake, kwani hata kabla ya kugombea uraisi alienda Butiama kwa Mwalimu ili kupata ridhaa yake. 
10. Katika uongozi wake amejutia maamuzi kadhaa aliyowahi kuyafanya, kwa mfano: 
  i. Kumpendelea baba mkwe wa mtoto wake katika ubinafsishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira. 
  ii. Kuchukua mkopo wa benki ya NBC kwa kutumia anuani ya Ikulu ili hali mkopo huo ulikua kwa ajili ya matumizi binafsi. 
 iii. Kuruhusu akaunti ya EPA (external payment account) baada ya kutamanishwa na wawekezaji walio jitolea kuchangia mfuko wa kampeni wa CCM. Lakini baadae EPA ilizaa madeni kwa nchi.
 
Nukuu niliyoipenda kutoka kwenye kitabu, Mheshimiwa Mkapa, anasema "Nitamuachia Mungu wangu na nyinyi kuamua ni tofauti gani nimeifanya humu duniani"
Asante kwa kusoma makala hii.  

Post a Comment

0 Comments