Ivi unafahamu kwamba tarehe zote katika mwaka mzima huambatana na maadhimisho
au sikukuu za kimataifa? Tarehe 31 Julai ni siku ya kimataifa ya wanamgambo wa
hifadhi za taifa Duniani. Wanamgambo hawa wanamajukumu ya kulinda hifadhi
dhidi ya ujangiri na kuzingatia maisha ya wanyama kama Tembo, Faru nk.
Siku hii ya kimataifa husimamiwa na International Ranger Federation (IRF). IRF
ni shirika lililoanzishwa tarehe 31 July 1992 huko nchini uingereza. Tanzania
ni miongoni mwa wanachama wa IRF.
IRF wana utaratibu wa kutoa tuzo zao kila baada muda wa miaka kadhaa.. Mnamo
mwaka 2018 Mgambo kutoka Tanzania, Wayne Lotter alitunukiwa tuzo ya Lifetime
Achievement Award (Tuzo ya heshima). Jina la tuzo pekee linaashiria kuna kazi
ya ziada aliifanya Mgambo huyo.
Ngoja nikujuze, Wayne Lotter alipoteza maisha yake akiwa katika harakati za
kupambana na majangiri hifadhini. Sasa kwa kuzingatia uduni wa mazingira ya
kufanyia kazi na vitendea kazi, IRF iliamua kumpa Mtanzania huyu tuzo ya
heshima! Tanzania ndio nchi inayoshikilia rekodi hii mpaka pale tuzo zingine
zitakapofanyika.
Nimekuandikia makala hii ili kuonesha na kutambua mchango wa Wanamgambo wa
hifadhi za Tanzania katika Utalii. Wakifanyia kazi zao katika mazingira
hatarishi na katika upungufu wa vifaa wanaipeperusha bendera ya Tanzania
katika uso wa dunia tarehe 31 July (World Ranger Day) na kuvutia watalii wengi
zaidi.
Asante kwa kusoma makala hii, bofya
hapa kufamu zaidi
kuhusu IRF na World Ranger Day.
0 Comments