Tabia 5 za watu wenye utajiri wa hisia.



Je, unafahamu kwamba kiwango cha hisia kinatofautiana kati ya mtu na mtu? Hisia ni utajiri pia. Sasa swali la msingi ni, utajiri wa hisia ni bora zaidi ya utajiri wa pesa/mali? Unaweza kujibu pesa ni bora zaidi! Lakini hauwezi kudharau mchango wa hisia katika ukuaji wa mtu

 Hizi ndizo tabia 5 za watu wenye utajiri wa hisia, ebu jipime uone uko wapi. 

 1. Wana mawazo chanya muda wote. 
Mtu mwenye utajiri wa hisia haogopi kuwazia mema kila kinachomzunguka. Katika mazingira tunayoishi ukiweza kubeba mawazo chanya juu ya kila mtu, maamuzi na tabia za watu basi utakua unaingia katika utajiri wa hisia. 
 2. Ni wawekezaji.
Sio kila uwekezaji unahitaji pesa. Inawezekana kabisa kuwekeza hisia zako kwa mtu mwingine. Uwekezaji wowote unahitaji kukua, sasa kadri hisia ulizowekeza kwa mtu mwingine zinavyozidi kukua(kumfanya asikie uwepo wako) hivyo ndivyo unavyozidi kukua pia. Ni matajiri wa hisia tu ndo wanaweza kuwekeza hisia zao. 
 3. Hawaogopi hasara.
Tunaweza kuchukulia mfano mdogo wa kuingia katika mahusiano. Ukiwa muoga wa kuumizwa huwezi kumkabidhi mtu hisia zako za kimapenzi. Lakini tajiri wa hisia haogopi kupata hasara katika uwekezaji wake wa hisia. 
 4. Wako salama muda wote.
Unajua kuteka benki na kuiba fedha sio rahisi kama tunavyoona kwenye filamu. Tajiri wa hisia ana benki yake ambayo inampa nywira(password) yule anayetakiwa. Tajiri wa hisia atawekeza hisia zake kwa watu sahihi bila kujua. Kwa nini? Siku zote watu wakiona hisia za mtu mwingine ziko juu sana hushindwa hatakuanzisha ukaribu. Kwa hiyo tajiri wa hisia yuko salama muda wote. 
 5. Ni watoaji.
Kuna tofauti kati ya utoaji na uwekezaji. Uwekezaji unategemea kupata chochote kama faida. Lakini kutoa hakuhitaji faida yoyote. Yule anaetoa hisia zake kwa ajili ya watu wengine siku zote hupata zaidi ya kile alichotoa bila kufahamu. Ngumu sio? Ndio, iko hivyo, matajiri wa hisia hujitoa sana katika hisia zao bila kutegemea malipo lakini ki uharisia kuna faida wanapata. Sisemi tufanye vitu bure, ila tambua ya kwamba kuna faida kubwa kwenye utoaji. 

Asante kwa kusoma makala hii, ni imani yangu kwamba umetambua uko upande gani, mafukara au matajiri wa hisia! 
Bofya hapa ku-SUBSCRIBE YouTube channel yetu.

Post a Comment

0 Comments