28 Agosti Na Harakati Za Mtu Mweusi "I Have A Dream"


Mnamo tarehe 28 Agosti, 1963, Marekani na dunia nzima ilishuhudia harakati kubwa za mtu mweusi katika kudai haki zake za msingi. Katika tarehe hii Martin Luther King, Jr aliongoza maelfu ya wanaharakati wengine nchini marekani kwa kufanya public speech iliyobaki katika masikio ya watu wengi duniani mpaka hii leo.

Moja ya vitu alivyoongelea ni ndoto yake ya kwamba siku moja mtu hatokuja kuhukumiwa kutokana na rangi ya ngozi yake na alienda mbali na kusema siku moja kiongozi mkuu wa Marekani atakuwa mtu mweusi, ambaye ni .


Sasa siku ya tarehe 28 Agosti ni kumbukizi ya speech hii maarufu iitwayo "I Have A Dream". Watu hukumbukia siku hii kwa kuvaa nguo nyeusi na nyeupe. Pia huendelea kuhubili kuhusu usawa wa watu bila kujali rangi ya ngozi kwa kuendesha kampeni iitwayo WAO (We Are One).

Nadhani hiki ni kitu cha muhimu ku-support kwa sababu matukio ya kushambuliwa kwa mtu mweusi yamekuwa mengi katika taifa la Marekani, taifa ambalo linaweza kuathiri hata nchi zinazoendelea kama Tanzania.


I have a dream that my four little children will one day live in a nation where they will not be judged by the colour of their skin, but by the content of their character...

Martin Luther King, Jr

Tazama speech hii kwa urefu zaidi hapa.