TalentSmart walifanya utafiti kwa watu zaidi ya milioni moja na kugundua kwamba asilimia kubwa ya watu tunakosa social awareness, hivyo ni muhimu sana kuwa makini katika mazungumzo ya kila siku. Yafuatayo ni maneno '5 ambayo watu wenye busara huyakwepa sana katika mazungumzo.
1. UMECHOKA!
Mtu aliyechoka siku zote anaoneka kuwa na macho mekundu na mazito, nywele zisizo na mpangilio, sura yenye makunyazi n.k. Huenda utamwambia mtu maneno haya kwa lengo la kumsaidia lakini baadhi ya watu wanaweza kuyachukulia kama dharau. Badala yake usiseme maneno ya moja kwa moja, unaweza kuuliza "Uko sawa?". Hapa sasa utaonekana ni mtu anayejali na anayependa kujulia hali watu wengine.
2. UMEPUNGUZA SANA UZITO.
Kama umekutana na mtu baada ya muda mrefu kisha ukamtamkia maneno haya inaweza kuleta shida ndani ya akili yake. Utamfanya avute picha ya mwili wake wa zamani na kujisikia vibaya ikiwa ni kweli kwamba alikua na mwili mbovu. Badala yake unaweza kumwambia "Umependeza sana". Maneno haya yatamfanya asifikirie ule mwili wake wa zamani na ajikite katika mwili wake wa sasa.
3. HATA HIVYO NI SAWA KWA UMRI WAKO!
Maneno haya yanamaanisha umemlinganisha na watu wengine kisha ukaona yuko sawa kutokana na umri wake ila hafui dafu kwa watu wengine duniani. Lakini kiuharisia watu hawapendi kulinganishwa na marehemu watarajiwa. Watu wanapenda kuwa vizuri kimpango na wanavyofikiri wao. Badala yake unaweza kusema "Uko vizuri". Maneno haya hayaleti comparison na watu wengine duniani.
4. KILA KITU NI JUU YAKO, AMUA UTAKAVYO.
Katika maisha ya kila siku mtu anaweza kukuomba umsaidie kuchangua baadhi ya vitu vinavyomhusu. Inawezekana pia huwezi kumfanyia chaguo lolote lakini badala ya kutumia maneno hayo unaweza kusema "Sina chaguo sahihi kati ya hayo, lakini kuna vitu naweza kushauri uvizingatie...". Hapo aliyekuomba ushauri atakuwa tayari kukusikiliza na atakuona mtu mwenye msaada kwake.
5. KAMA AMBAVYO NIMESHAKUAMBIA...
Binadamu wote tunaudhaifu wa kusahau. Ukitumia maneno haya utamfanya anayekusikiliza kuonekana mpumbavu, msahaurifu na mbishi. Unayesema maneno haya utaonekana mwenye dharau na kujiona mkamilifu (si inajua people are complicated). Badala yake tafuta njia sahihi ya kukumbushia kile ulichokisema hapo kabla bila kuwafanya wanaokusikiliza wajione wasahaurifu.
Visit our socials