Lifestyle: Fahamu Mr. Africa Alichokisikiliza, Kutazama na Kusoma Wiki Hii | #001 | No Video Review

...

Inakuaje? Ni Mr. Africa hapa wa Bona vision production. Ee bwana kutokana na kutokuwepo kwa video review kutoka kwetu kwa wiki hii kama ilivyozoeleka, nimeamua kufanya jambo la kitofauti ili tuendelee kuwa connected.

Ningependa ku-share mambo niliyofurahia kufanya katika wiki inayokamilika leo hii (30th August – 5th September).

Ni mambo matatu; nilicho-enjoy kusikiliza, nilicho-enjoy kutazama na nilicho-enjoy kusoma.

  • Nimesikiliza album ya Johnny Drille iitwayo Before We Fall Asleep. Ni moja ya album mpya na bora za mwaka huu (haina hata mwezi tangu itoke). Nimefurahia utunzi, ujumbe alioweka na ubora wa audio production. Mziki uliotawala kwenye album hii ni ‘Live Music’. Sijajutia kuipa sikio langu. Itapendeza kama utaisikiliza na unipe feedback yako.
  • Nimetazama All it takes is 10 mindful minutes by Andy Puddicombe. Andy Puddicombe ni monk. Kupitia talk yake nimejifunza maana halisi na umuhimu wa meditation. Aliuliza swali zuri sana mwanzoni wa talk yake: When did you last take any time to do nothing? Kupitia swali hili Andy Puddicombe amenijengea stadi moja nzuri sana ya kutumia kuepuka msongo wa mawazo. Msikilize pia naamini itakusaidia!
  • Nimesoma What Matters More Than Your Talents Speech by Jeff Bezos. Jeff Bezos (mmiliki wa Amazon) kupitia chapisho hili ametofautisha kati ya Talent na Choice (unachotakiwa kufanya siku hadi siku). Nimejifunza kitu kutoka kwake. Kasome pia.

Hatujaweza kuandaa video review kwa wiki hii kutokana na ratiba zingine za maisha tuliyonayo kila siku. Lakini ni imani yetu kwamba kupitia blogpost hii tutaendelea kuwa pamoja.

Tuandikie comment kama ungependa kusikia zaidi kuhusu ninachokifanya (Mr. Africa) kila wiki. Uwe na wakati mwema, Chao!

Post a Comment

0 Comments