Star wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameupiga mwingi sana ndani ya mwezi November! Haya ni baadhi ya matukio. Harmonize alitoa album yake mpya ya "High School" ndani ya mwezi November. Harmonize huyu huyu alikamilisha Music Tour yake nchini Marekani ndani ya mwezi November. Lakini pia ali-trend sana kwa mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari kuhusu uhusiano wake na Diamond Platnumz mara baada ya kutua nchini Tanzania akitokea Marekani. Isitoshe Harmonize amefanikisha tamasha kubwa la "Ibraah Homecoming" mkoani Mtwara kwa ajili ya msanii wake, Ibraah.
Mwezi November unakuwa mwezi bora sana kwake kwa kufanikiwa kuongoza orodha wa wasanii walioongeza YouTube subscribers kwa kasi zaidi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.
Msimamo wa ongezeko la subscribers kwa wasanii wa Tanzania ndani ya mwezi November 2021 upo kama ifuatavyo.
# | Msanii | Ongezeko |
---|---|---|
1 | Harmonize | 80K+ |
2 | Diamond Platnumz | 70K+ |
3 | Mbosso | 70K+ |
4 | Rayvanny | 70K+ |
5 | Alikiba | 40K+ |
6 | Lava Lava | 30K+ |
7 | Zuchu | 30K+ |
8 | Macvoice | 28K+ |
9 | Marioo | 24K+ |
10 | Nay wa Mitego | 16K+ |
Bona vision production tunaandaa orodha hii kila mwezi hivyo kaa karibu na mitandao yetu ya kijamii ili usikose kufahamu tutakacho kiaandaa.
1 Comments
Kondeboy For everybody
ReplyDelete