Fik Fameica Ft Harmonize - Champino | Hakuna na Hajatokea Msanii wa Kumfunika Harmonize Kwenye Hili.

...

Inakuaje? Ni Mr. Africa hapa wa Bona vision production. Msanii wa Bongo Fleva Harmonize ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa msanii Fik Fameica kutoka Uganda uitwao “Champino”. Ikumbukwe kwamba sio mara ya kwanza kwa Fik Fameica kufanya kazi na msanii wa Bongo Fleva. Kumbukumbu zangu zinakumbusha ngoma aliyofanya na Rayvanny, “Mwaga” miaka mitatu nyuma - 2018.

Binafsi nauona mwaka 2022 ukianza vyema sana kwa wasanii watanzania na Afrika mashariki kiujumla. Kwenye wiki ya kwanza ya mwezi Januari tumeshuhudia ngoma kubwa ya The Ben na Diamond Platnumz ikiachiwa na kufanya vizuri. Harmonize na Fik Fameica wamekuja pia na ngoma yao ndani ya wiki ya kwanza ya Januari.

Nimeipa sikio ngoma hii ya champino na ninachokiona ni kwamba Harmonize ameamua kukazania jambo lake la siku zote. Kwamba wasanii wa Tanzania watatoboa kimataifa kirahisi kwa kuimba ngoma zao kwa kingereza. Ila naona sio kingreza tu bali ni kingereza kinachoimbika kama ambavyo amekuwa akifanya yeye (Harmonize) siku zote.

Ngoma hii ya champino ni inspiration kwa vijana wote wapambanaji. Ujumbe ni mzuri sana hasa mwanzoni mwa mwaka kama hivi. Fik Fameica “King Kong” anakwambia “man I suffered too long, I never gave up!”. Kwa upande wa Harmonize inspiration songs sio issue kabisa.

Mpaka sasa Harmonize ndiye msanii pekee (katika wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa) ambaye ana hitsongs nyingi zenye ujumbe wa inspiration. Ngoma kama Hainistui, Jeshi, Wapo, Usia n.k. Hivyo niliposikia verse ya mwanzo ya Fik Fameica "King Kong" nilielewa tu kwamba Harmonize kapiga verse nzuri. Baada ya kusikiliza mawazo yangu hayakukosea. Mashairi ni yenye ujumbe na vibe la kuchezeka pia. Hii inampa Harmonize utofauti sana hapa Bongo.


Post a Comment

0 Comments