The Ben Ft Diamond Platnumz - Why | Kama Bado Unajiuliza Diamond Anaimba Nini, Soma Hii.

...

Inakuaje? Ni Mr. Africa hapa wa Bona vision production. Ikiwa ni siku za mwanzo kabisa za mwaka huu 2022 Diamond Platnumz na The Ben kutoka Rwanda wametusogezea ngoma yao mpya kabisa "WHY". Nimepata nafasi ya kuisikiliza mapema kabisa na hapa nipo kukupa feedback ya awali ya mashairi na utamu wa ngoma hii.

Ukiachilia mbali ngoma ya "Unaanzaje", katika kipindi chote cha mwaka 2021 Diamond Platnumz ajafanya ngoma ya miondoko hii. Ngoma nyingi zimekuwa ni za kuchezeka zaidi. Isitoshe kuna vionjo flani vya Bongo Fleva Nilikuwa na vi-miss kutoka kwa Diamond Platnumz especially kwenye ushairi mzuri wa kiswahili. Wengine tuliona kama mziki wa Diamond Uko maji ya jioni!

Lakini kwa alichokifanya katika ngoma hii ya "Why" naweza kusema Diamond Platnumz bado ana safari nzuri na ndefu sana katika mziki wake. Kwa verse aliyoifanya kwenye ngoma hii naitabiria makubwa sana kama ilivyo kawaida yake. Kizuri zaidi ni kwamba nyimbo ni international na ina-connect East Africa kiujumla.

Diamond Platnumz na The Ben wamefanya vyema sana kwenye ngoma hii. Naona kabisa Diamond Platnumz akirudi kwenye line ya Bongo Fleva kwa miondoko hii ndani ya mwaka 2022.

Yapi ni maoni yako njuu ya ngoma hii? Tukutane kwenye post nyingie. Hii ni Bona Vision Production!.


Post a Comment

0 Comments