Star wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz ameufunga mwaka kwa kishindo kikubwa mara baada ya kuongoza tena katika ongezeko la subscribers ndani ya mwezi December 2021. Licha ya rekodi hiyo Diamond Platnumz amefikisha idadi ya subscribers milioni sita (6) kwenye mtandao wake wa YouTube.
Aidha, wasanii wa record label ya Wcb Wasafi wamefanya vizuri sana katika orodha za mwaka 2021 tulizozitoa hapa.
Msimamo wa ongezeko la subscribers kwa wasanii wa Tanzania ndani ya mwezi December 2021 upo kama ifuatavyo.
# | Msanii | Ongezeko |
---|---|---|
1 | Diamond Platnumz | 140K+ |
2 | Rayvanny | 60K+ |
3 | Zuchu | 60K+ |
4 | Harmonize | 40K+ |
5 | Lava Lava | 40K+ |
6 | Mbosso | 30K+ |
7 | Macvoice | 26K+ |
8 | Mabantu | 22K+ |
9 | Alikiba | 20K+ |
10 | Marioo | 19K+ |
Bona vision production tunaandaa orodha hii kila mwezi hivyo kaa karibu na mitandao yetu ya kijamii ili usikose kufahamu tutakacho kiaandaa.
0 Comments