Star wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz ameufungua mwaka 2022 kwa kishindo kikubwa. Hii ni mara baada ya kuongoza katika ongezeko la YouTube subscribers ndani ya mwezi January mwaka 2022.
Licha ya rekodi hiyo, mtando wa YouTube charts umeripoti mapema mwaka huu kwamba Diamond Platnumz ndiye msanii namba tatu kwenye orodha ya wasanii walioko kusini mwa jangwa la Sahara, waliotazamwa zaidi ndani ya mwaka 2021 kwenye mtandao wa YouTube.
Msimamo wa ongezeko la subscribers kwa wasanii wa Tanzania ndani ya mwezi January 2022 upo kama ifuatavyo:
# | Msanii | Ongezeko |
---|---|---|
1 | Diamond Platnumz | 120K+ |
2 | Harmonize | 70K+ |
3 | Rayvanny | 70K+ |
4 | Zuchu | 50K+ |
5 | Alikiba | 40K+ |
6 | Mbosso | 30K+ |
7 | Killy | 28K+ |
8 | Marioo | 23K+ |
9 | Lava Lava | 20K+ |
10 | Jux | 18K+ |
Bona vision production tunaandaa orodha hii kila mwezi hivyo kaa karibu na mitandao yetu ya kijamii ili usikose kufahamu tutakacho kiaandaa.
0 Comments