Top 10: Diamond Awavuta Wadada Wanne Kwa Mpigo. Hii Haijawahi Kutokea! | Subscribers Gain June 2022

...

Diamond Platnumz amepania kweli kweli mwaka huu! Ameongoza orodha ya ongezeko la subscribers hapa Tanzania kwa mwezi wa sita mfululizo.

Katika orodha ya mwezi huu tumeshuhudia utofauti mkubwa. Kwa mara ya kwanza wasanii wa kike wanne wameingia kwenye orodha hii. Saraphina, Lulu Diva, Anjella na Zuchu. Saraphina na Lulu Diva wameingia kwenye orodha hii kwa mara ya kwanza kabisa. Diamond Platnumz ambaye ndiye kinara ya orodha hii ni kama amewavuta wasanii wakike wengi zaidi kwa mpigo na yeye akiwa kinara. Hakuna kinara mwingine aliyewahi kufanya hivi.

Msimamo wa ongezeko la subscribers kwa wasanii wa Tanzania ndani ya mwezi June 2022 upo kama ifuatavyo:

# Msanii Ongezeko
1 Diamond Platnumz 110K+
2 Rayvanny 100K+
3 Harmonize 50K+
4 Marioo  36K+
5 Mbosso 30K+
6 Zuchu 30K+
7 Anjella 17K+
8 Stamina 16K+
9 Lulu Diva 15K+
10 Saraphina 14K+

Bona vision production tunaandaa orodha hii kila mwezi hivyo kaa karibu na mitandao yetu ya kijamii ili usikose kufahamu tutakacho kiaandaa.

Post a Comment

0 Comments